Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya ukaguzi wa masuala ya kazi na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.

Mavunde alianza ziara hiyo katika shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM) ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na kutoa maagizo kwa Menejimenti ya Uongozi wa Shule hiyo kutoa mikataba kwa wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini kinavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kuagiza Taasisi za Serikali kuchunguza malalamiko juu ya unyanyasaji kwa wafanyakazi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa menejimenti.

Mavunde pia alitembelea Kiwanda cha China Paper Corporation ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na kuiagiza Menejimenti ya Kiwanda hicho kuhakikisha sheria za Kazi zinafuatwa kwa kutoa Mikataba kwa wafanyakazi wote na kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa ikiwemo usalama wa mazingira ya kufanyia kazi.

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua nyaraka mbalimbali alipotembelea Kiwanda cha China Paper Corporation.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua kiwanda cha China Paper Corporation.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akizungumza katika kiwanda cha China Paper Corporation.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...