Dodoma Mjini Anthony Mavunde wampongeza Mh. Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli kwa uamuzi wake kuhamishia Makao makuu ya Serikali Dodoma na hivyo kuongeza fursa za kiuchumi katika mkoa wa Dodoma kupitia uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali zitakazotolewa.
Wakizungumza leo katika kipindi cha 360 cha Clouds TV wamesema uamuzi huo ni fursa muhimu kwa wanadodoma ni vyema wakaitumia ipasavyo.Aidha wamempongeza Mh. Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kuivunja CDA na kurudisha mamlaka ya utawala wa ardhi chini ya Manispaa ya Dodoma na kubadilisha mfumo wa umiliki ardhi kutoka katika upangaji(Lease Ground) kwenda kwenye mfumo wa hati ya umiliki.
Wamesema kupitia mfumo huo Dodoma itapata fursa ya kuvutia zaidi wawekezaji wa muda mrefu tofauti ilivyokuwa awali.
Aidha Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ameelezea mipango mikubwa ya ukuzaji mji wa Dodoma ikiwemo uharakishwaji wa huduma ya vibali vya ujenzi,upimaji wa mae uboreshwa wa miundombinu na huduma za kijamii ili viende sambamba na ukuaji wa haraka wa mji wa Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...