Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amana Bank, Bw. Bakari Kisuda akizungumza na Waandishi wa Habari Waislamu jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Kiislamu wa Afrika ya Mashariki (MJEA) kwa kushirikiana na kampuni ya KO Innovates zimeendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari vya Kiislamu hapa nchini.
Mwenyekiti wa MJEA, ABUOBAKARI FAMAU,amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari wanaotoka kwenye vyombo hivyo vya habari ili waweze kuendana na mazingira ya sasa ya tasnia ya habari.
FAMAU ameongeza kuwa vyombo vya Kiislamu vina wajibu kubwa sana kwa jamii na hivyo kuna haja ya kukumbushana juu ya wajibu huo.
nae Khadijah Omar amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwakutanisha waandishi wa habari wa vyombo vya Kiislamu na kubadilishana uzoefu.
Zaidi ya washiriki 25 wamepatiwa mafunzo hayo ambayo yatafanyika Novemba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Tangaza House jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amana Bank,Bakari Kisuda akizungumza na Waandishi wa Habari Waislamu jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Kiislamu wa Afrika ya Mashariki (MJEA)
Waandishi wa Habari wa Mashirika ya Kislamu nchini wakifatilia hotuba ya mgeni Rasmi kwa makini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...