TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa maandalizi ya vifaa kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa madiwani unaofanyika katika kata 43 yamekamilika na awamu ya pili ya vifaa vitaanza kusafirishwa leo Ijumaa kwenda katika kata husika.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Kailima Ramadhani, alisema kwamba vifaa vitakavyosafirishwa kuanzia kesho ni maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo, makarani waongozaji pamoja na mfano wa karatasi za kupigia kura.
Alisema awamu ya kwanza ya kusafirisha vifaa ulifanywa na tume wakati wa mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi ambayo yalifanyika mjini Dodoma ambavyo vilitumika wakati wa uteuizi wa wagombea udiwani katika kata zote.
“Napenda kuwahakikishia umma kwamba tume imejipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi huu na maandalizi ya kupeleka vifaa katika husika yako vizuri na awamu ya pili ya upelekaji wa vifaa itapaelekwa kesho (leo),”alisema Ramadhani.
Alisema awamu ya tatu ya usafirishaji wa vifaa itahusisha vifaa vichache ambavyo ni karatasi za kupigia kura pamoja na fomu za kutangazia washindi ngazi ya kituo na ngazi ya kata.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...