Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKUU wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo
kigamboni,Profesa , Shadrack Mwakalila
ameagiza wanafunzi wa chuo hicho, waliojiunga katika mwaka wa Masomo wa
2017 kutojiusisha na masuala ya siasa pindi wanapokuwa chuo na badala yake
wazingatie katika suala zima la taaluma ili waweze kupata kile kilicho
wapeleka chuoni hapo.
Profesa Mwakalila amesema hayo alipokuwa akizungumza na
wanafunzi wa Mwaka wa kwanza juu ya nini wanatakiwa kufanya wakiwa chuoni hapo
na kutambua nini cha msingi kilichowaleta.
"Hapa sio mahali pakufanya Siasa ni sehemu mliyokuja
kuchukua taaluma, kamwe msikubali wanasiasa kuwatumia kwa ajili ya maslahi yao
kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmepoteza lengo ambalo limewaleta hapa katika
kufanikisha malengo yenu ya kitaaluma"amesema Profesa Mwakalila.
Profesa Mwakalila ameongeza kuwa kama wanavyojua chuo hicho
kimetokana na Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius .K. Nyerere hivyo wanapaswa
kufuata maadili na kuwa waadilifu ili kumuenzi muasisi Baba wa Taifa ambaye
alikuwa na ndoto ya kuwa sehemu hiyo iweze kupika viongozi wenye maadili mema
kwa Taifa hili.
alimaliza kwa kutoa wito kwa wote waweze kukazana katika
masomo yao hili waweze kuwa alama ya chuo hicho pindi wanapomaliza masomo yao
na kufika hapo kwao isiwe majuto.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam,Profesa. Shadrack Mwakalila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo hicho wa Mwaka wa kwanza ambao wamechaguliwa katika muhula wa Masomo 2017 kwa ngazi ya Cheti, Astashahada na Shahada juu ya umuhimu wa kufuata Maadili.
Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akikazia jambo juu ya kuwa na maadili shuleni
Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...