Leo Jumatatu Rais wa Cameroon Paul Biya, anaadhimisha miaka 35 uongozini na kumfanya kuwa Rais aliyehudumu kwa miaka mingi zaidi barani Afrika.

Bwana Biya aliingia kwa mara ya kwanza uongozini mwaka 1982, wakati taifa hilo lililikuwa chini ya mfumo wa utawala wa chama kimoja.
Hata hivyo, licha ya taifa hilo kwa sasa liko katika mfumo wa uongozi wavyama vingi vya kisiasa, amefaulu kusalia mamlakani kwa miaka hii yote.

Mnamo mwaka 2011, baada ya katiba ya taifa hilo kunayiwa mabadiliko yenye utata ya kumruhusu kuwania kiti cha Urais tena, alifaulu kushinda tena uchaguzi mkuu kwa asilimia 78 ya kura zote zilizopigwa na kusalia mamlakani kwa miaka mingine saba.

Ushindi huo mkubwa, uliwafanya wakosoaji wake wengi kuhoji na kushuku uhalali wa uchaguzi huo.Bwana Biya ni sehemu ya kundi la viongozi kadhaa Afrika, ambao wametawala mataifa yao kwa zaidi ya miaka 30: Wao ni pamoja na Robert Mugabe wa Zimbabwe na Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa taifa dogo la Equatorial Guinea, ambao wangali wakishikilia mamlaka.

Bwana Biya mwenye umri wa miaka 84, na ambaye wakosoaji wake wanamtuhumu kwa kuongoza taifa kiimla, anatarajiwa kuwania tena kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu mwaka ujao wa 2018.
Unaweza kupata mengi kumhusu Bw. Biya.

Chanzo: BBC Swahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...