Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Modest Apolinary kupeleka Wakaguzi wa ndani wa Hesabu za Serikali Kata ya Mgusu ili wakakague na kujiridhisha na mapato na matumizi ya fedha mbalimbali katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Mgusu na Mtaa wa Machinjioni Wilayani Geita.

Mheshimiwa Robert amesema hayo wakati wa ziara yake Halmashauri ya Mji Geita yenye lengo la kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati ambapo baada ya uzinduzi kufanyika wananchi wa mtaa wa machinjioni walimueleza kero ya kutopata taarifa ya mapato na matumizi ya michango wanayochangia kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa muda mrefu katika mtaa na kata ya Mgusu.

Akijibu kero hiyo Mkuu wa Mkoa amesema "Kama kuna kiongozi wa mtaa au Kata amekula fedha za wananchi hafai kuwa kiongozi serikali itamchukulia hatua kali za kisheria na atarejesha fedha hizo!, Mkurugenzi leta timu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ikague na kujiridhisha kama kuna fedha yoyote iliyochukuliwa pasipo maelezo yanayojitosheleza hatua zichukuliwe haraka kwa wote watakaobainika kuhusika". 

 Mheshimiwa Robert ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanyike kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 kisha apate taarifa hiyo ofisini. Akiwa katika Halmashauri hiyo Mkuu wa Mkoa amepongeza jitihada zinazofanywa na wananchi za kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo licha ya kuwepo changamoto nyingi katika maeneo yao.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananfunzi wa Shule ya Msingi Shinamwendwa (Halmashauri ya Mji Geita) alipokwenda kushiriki kuchmba msingi wa ujenzi wa nyumba pacha ya Walimu shuleni hapo.
Akina mama wa mtaa wa Machinjioni Kata ya Mgusu Halmashauri ya Mji Geita wakishiriki katika ujenzi wa jengo la utawala kwa kubeba maji kupeleka eneo la mradi.Wananchi wwameamua kujenga Shule ya Sekondari kwa kuwa Kata hiyo haina hata shule moja hivyo watoto wanaofaulu ulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu ya Sekondari katika Kata za jirani.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Mgusu baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati Halmashauri ya Mji Geita.Kata ya Mgusu inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na Shule ya Sekondari. 
Mhandisi Modest Apolinary Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita kitoa ufafanuzi kuhusu ramani ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mgusu kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel kulia ni Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...