Serikali imeahidi kutoa bure pembejeo za kilimo kwa wakulima mbali mbali wa zao la pamba mkoani Singida kuanzia msimu huu wa kilimo ikiwa ni moja ya juhudi za kuhamasisha na kufufua kilimo hicho mkoani hapa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga ameeleza hayo juzi katika vijiji vya Kinyangiri na Lyelembo wilayani Mkalama katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili kuhimiza Kilimo cha pamba mkoani Singida.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Biosustain iliyopo mjini hapa imepewa jukumu la kuleta na kusambaza mbegu na madawa yote yahusuyo kilimo cha pamba bure na kwamba gharama ya pembejeo hizo italipwa na Serikali.
Kutokana na hilo, Mkurugenzi huyo amewataka Wakulima kutumia vyema fursa hiyo kwa kulima mashamba makubwa zaidi lakini pia kwa kuzingatia tija na ubora wa pamba. Amesema kuwa Wakulima wataweza kufanya hivyo tu iwapo pia watawatumia kikamilifu wataalamu wao wa kilimo na kufuata Kanuni na Taratibu za kilimo bora.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi mmoja kati ya wa wakulima wa Pamba wa kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama kilo kumi za mbegu za zao la pamba zilizotolewa bure na Serikali kwa wakulima hao. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga.
Mkulima wa Pamba Bi Johari kutoka kijiji cha Kinyagiri Wilayani Mkalama akibeba mbegu za Pamba kilo kumi alizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi, mbegu hizo zimetolewa bure kwa wakulima wa Pamba Mkoa wa Singida.
Mama Devid Mkulima wa Pamba wa Kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama akijifunza kwa vitendo namna ya kuandaa kamba inayotumika kuonyesha vipimo vya upana na urefu katika kupanda pamba badala ya kilimo cha mazoea cha kumwaga mbegu bila kufuata kipimo chochote.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...