NA ESTOM SANGA-TASAF

Vikao Kazi vya Serikali na Wadau wa Maendeleo vinaendelea kufanyika mjini Dar es salaam kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Mapitio hayo ni utaratibu wa kawaida wa kupima mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaohudumia kaya za walengwa zipatazo MILIONI MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

Washiriki wa vikao kazi hivyo vinavyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za makao makuu ya TASAF mjini Dar es salaam, ni pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali kutoka Wizara ya Fedha, serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Ofisi ya Rais,Benki ya Dunia,UNICEF,Shirika la Misaada la Ireland,na Shirika la Misaada la Uingereza DFID.

Wengine ni kutoka UNDP,USAID ,ILO,Fundacion Capital,Brac Tanzania, SVPO Zanzibar,PO- RALG Dodoma, VPO-DOE,MOHCDGEC ,Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Ujenzi,na Wizara ya Kilimo. TASAF imekuwa ikishirikiana na Wizara na wadau hao wa Maendeleo katika kutekelezaji jitihada za serikali za kupunguza adha ya umaskini kwa wananchi wanaoishi katika umasikini uliokithiri.

Vikao kazi hivyo ambavyo vinafanyika baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa Mpango pia vinajadili muundo wa Awamu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya masikini na vitahitimishwa hapo kesho na kisha siku inayofuata andiko la pamoja la mapendekezo ya kuboresha utekelezaji wa Mpango litafikiwa na kisha kuwasilishwa serikalini kupata idhini.
Moja ya kundi la watendaji wa serikali, wadau wa maendeleo na TASAF wakiendelea na mjadala.
Pichani, baadhi ya maafisa wa TASAF na wadau wa maendeleo wakiendelea na majadiliano juu ya masuala ya uboireshaji wa shughuli za mpango.
Pichani ya juu na chini ni wajumbe wa kikao kazi cha maafisa wa TASAF na wadauy wa maendeleo wakiwa kwenye moja ya kumbi kujadili mafanikio na changamoto wa Mpango wa kunusuru kaya masikini.
Pichani baadhi ya washiriki wa vikao kazi kati ya wadau wa maendeleo, TASAF na serikali wakiendelea na mjadala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...