SHIRIKA la PELUM Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kupitia linatarajia kutoa hati miliki za kimila 795 kwa wananchi wa Vijiji vya  Ugesa, Isaula, Magunguli na Usokami na Mukungu waliopimiwa ardhi zao kupitia Mpango wa Matumizi bora ya ardhi.

Hayo yamesemwa jana (juzi) Wilayani Mufindi na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Leonard Jaka  wakati wa zoezi la upitishaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi uliofanywa katika kijiji hicho na Shirika la PELUM Tanzania kupitia mradi wa Ushiriki wa wananchi katika Sekta ya Kilimo (CEGO).

Jaka alisema Wananchi wa kijiji cha Makungu pamoja na vijiji jirani katika Halmashauri hiyo kuchangamkia fursa hiyo ya kupima ardhi zao ili kuweza kuepekana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiathiri shughuli za maendeleo ya wananchi Wilayani humo.

Jaka alisema mpango huo ni muhimu kwa kuwa unatoa kipaumbele kwa wajane, wagane, walemavu, wazee na watu wenye kipato cha chini kupata hati miliki ya ardhi na hivyo aliwataka wananchi ambao hawajapimiwa ardhi zao wahakikishe wanajipanga ili waweze kufikiwa na mpango huo.

“Kupimwa kwa ardhi zenu kutasaidia kuepukana na migogoro ya ardhi, kujihakikishia ulinzi wa ardhi,kuwa na umiliki halali wa kisheria wa ardhi, kuongezeka kwa thamani ya ardhi pamoja na kurahisisha upatakanaji wa mikopo kwa kuweka ardhi yako kama dhamana,” alisema Jaka.
 Mmoja wa wajumbe toka Kamati ya Usimamizi wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi (VLUMC) ya Kijiji cha Makungu akiwasilisha Mpango pendekezwa wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji hicho wakati wa Mkutano wa pamoja uliojadili na kupitisha Mpango wa Matumizi bora ya ardhi katika Kijiji hicho. Mafunzo hayo yaliyofanyika juzi Kijijini hapo yalifadhiliwa na Shirika la PELUM Tanzania. 
Mwanasheria kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Mufundi, Method Msokeve akiwasomea wananchi wa Kijiji cha Mukungu Wilayani humo sheria ndogondogo zitakatumika wakati wa mipango mbalimbali ya matumizi ya ardhi Wilayani humo. Mafunzo hayo yaliyofanyika juzi Kijijini hapo yalifadhiliwa na Shirika la PELUM Tanzania. 
 Timu ya wataalamu toka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, na Wafanyakazi wa Shirika la PELUM Tanzania, pamoja na Viongozi wa Serikali za Vijiji vya Kiyowela, Idete na Makungu alama ya Mipaka inayotenganisha vijijiji hivyo kabla ya kufanyika kwa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji cha Makungu. Mafunzo hayo yaliyofanyika juzi Kijijini hapo yalifadhiliwa na Shirika la PELUM Tanzania.

Baadhi ya vibao vilivyowekwa katika baadhi ya maeneo ya kijiji cha Mukungu yakionesha mgawanyo wa matumizi ya ardhi katika kila eneo husika. Mafunzo hayo yaliyofanyika juzi Kijijini hapo yalifadhiliwa na Shirika la PELUM Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...