SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

WIZARA YA HABARI UTALII UTAMADUNI NA MICHEZO


Tel: 0255 24 2237325/0255 24 223 7313                          Idara ya Habari Maelezo
Fax: 0255 24 2237314 P.O. Box 2754
maelezozanzibar@hotmail.com,  maelezozanzibar@gmail.com                                                   

                     
Gazeti la Mwananchi la toleo Nam. 6330 la Jumapili Novemba 26, 2017 habari yake kuu inasema  “Butiku: Katiba Z’bar inataka Umoja wa Kitaifa, isipuuzwe”.
Taarifa hii haikuzingatia weledi, imejiegemeza katika ushabiki.
Ukweli ni kwamba hakuna katiba iliyopuuzwa  Zanzibar kama anavyodai Bwana Joseph Butiku. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeundwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 inaeleza bayana muundo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Tunamshauri Mzee Butiku akasome vizuri Katiba ya Zanzibar. Nafasi ya Makamu wa kwanza wa Rais ipo, haijafutwa. Sehemu ya Pili ya Katiba kifungu cha 39 kinazungumzia Makamu wawili wa Rais Zanzibar.
Katika kifungu cha 39 A (1) cha Katiba ya Zanzibar kinazungumzia kuachwa wazi kwa nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
Kifungu hicho kinasema;
Endapo, Ndani ya siku Saba mara baada ya Rais kushika madaraka, Chama kinachostahiki kutoa Makamu wa Kwanza wa Rais, kitashindwa kuwasilisha kwa Rais jina la uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais, Rais bila ya kujali masharti ya kifungu cha 39(1) na (3) cha Katiba, atawacha wazi nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kuteua Makamu wa Pili wa Rais.
Tunamshauri Mzee Butiku asome kwa umakini Kifungu cha 42(A) na vifungu vyengine vya Katiba ya Zanzibar.

Imetolewa na :-
Dk. Juma Mohammed Salum
KNY
Mkurugenzi
Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar
Zanzibar
26, Novemba, 2017













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...