Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linakanusha Taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikiwataka Wateja kununua Umeme kwa wingi kutokana na zoezi linaloendelea la kubomoa Ofisi za Makao makuu ya TANESCO hivyo kupelekea kuathirika kwa mfumo wake wa LUKU.
Tunaomba Wateja wetu wapuuze taarifa hiyo, kwani TANESCO kama ilivyobainisha katika taarifa ya awali , huduma zote za umeme ikiwemo ya manunuzi ya LUKU zitaendelea kama kawaida .
Tutaendelea kutoa taarifa kila inapohitajika.
Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: -
Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd
twitter.com/tanescoyetu
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Novemba 27, 2017
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...