Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera ameibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika jumapili.

Bi Bujinginya, mama wa watoto wawili ambaye anaungana na washindi milioni 130 wa Tatumzuka amesafirishwa kwa ndege kutoka Ngara kuja Dar es Salaam ili kuchukua pesa yake ya ushindi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Mikocheni.

Baada ya kushinda mara chache katika droo ya kila saa, alipata msukumo wa kuendelea kucheza bila kukata tamaa. "Baada ya kuishi kwa kutafuta pesa ya mlo kila mwezi na miezi mingine bila pesa, Kiukweli sikujua itakavyokuwa ikifika Januari. Nimefurahi sana kwamba sasa naweza kutembea kwa kujiamini tena baada ya ushindi huu’ alikiri Bi Bujinginya.

Pia katika tukio la kukabidhi zawadi kwa mshindi alikuwepo Bwana Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.Dhamira ya Tatu Mzuka ya kubadilisha maisha ya watu haijabadilika ambapo zimebaki siku chache ili ichezeshwe droo kubwa ya Supa Mzuka jackpot ya milioni 150 jumapili ijayo. Tarehe 19 Novemba saa 3:30 usiku Mtanzania mmoja ataondoka na kitita cha milioni 150.

"Kila mtu ambaye umecheza tangu Tatumzuka izinduliwe na kutumia kuanzia shilingi 500 tu kupitia MPESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY, umeingia katika droo hii ambapo unaweza kujishindia milioni 150," alielezea mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba.

Bi Mutahaba aliwahimiza watanzania kuendelea kucheza, akisisitiza kwamba bado washiriki hawajachelewa kujiwekea nafasi ya ushindi huo wa kihistoria.
Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi Bi.
Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera alieibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika mwishoni mwa wiki
Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi,Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...