Tanzania Media Foundation (TMF) imeipatia ruzuku ya shilingi milioni 112 Radio Habari Njema ya Mbulu Mkoani Manyara, kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi ili waibue kero, changamoto, mafanikio na kuandika kwa wingi habari za wananchi hasa waliopo Vijijini.
Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura, akizungumza mjini Babati wakati wa zoezi hilo, alisema vyombo vya habari ni mhimili usio rasmi ambao umekuwa ukiibua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo za maji, elimu, afya na mengineyo ambayo yakipatiwa ufumbuzi jamii inapata furaha.
Sungura alisema kupitia ruzuku hiyo, hii ni mara ya nne kupatiwa ruzuku na TMF na mara zote wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kuandaa vipindi vyenye maslahi ya wananchi. Alisema kupitia vipindi vilivyoandaliwa na redio hiyo haki za watoto na wanawake zimepatikana kwa ufadhili wa TMF.
Alisema kwa kuandika habari za jamii ikiwemo mafanikio, kero, ukosefu wa maji, vyoo, shule na mambo hayo yakapatiwa ufumbuzi wananchi hupata furaha baada ya mafanikio hayo. Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga ameipongeza TMF kwa kuiwezesha Redio Habari Njema, ambayo imekuwa inashirikiana na serikali katika kuchochea maendeleo ya jamii kupitia habari wanazozitangaza.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga (kulia) akishuhudia utiwaji sahihi wa kupatiwa shilingi milioni 112 ambazo ni fedha za ruzuku kwa Redio Habari Njema ya Mbulu zilizotolewa na Tanzania Media Foundation (TMF) mjini Babati, (katikati) ni Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura na Mhasibu mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu, Padri Anthony Lagwen
Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF) Ernest Sungura akizungumza mjini Babati wakati wa zoezi la kupatiwa fedha za ruzuku ya shilingi milioni 112 kwa Radio Habari Njema ya Wilayani Mbulu.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa Mkoa wa Manyara, Joseph Lyimo akizungumza kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna ya kuomba fedha za ruzuku Tanzania Media Foundation (TMF) Mjini Babati.
Waandishi wa habari wa Mikoa ya Manyara na Arusha, wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna ya kuomba fedha za ruzuku kupitia Tanzania Media Foundation (TMF) mjini Babati.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...