NA BASHIR NKOROMO.

Kundi la Tanzania One Theatre (TOT Plus), limo kambini Wanamuziki wake wakijifua vikali katika mazoezi ya nyimbo tatu ambazo kundi hilo litaziipua hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya nyimbo hizo, Mkurugezi wa TOT Plus inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gasper Tumaini amezitaja nyimbo hizo kuwa ni 'Tumuunge mkono JPM', 'Amani ya Tanzania' na Hongera awamu ya tano'.

Tumaini amsema, wimbo wa 'Tumuunge mkono JPM' ni wa kuwahamasisha Watanzania popote walipo kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika vita ya uchumi anayoongoza kwa kuhakikisha inaziba mianya inayotishia upotevu au matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

"Kama unavyoona Rais tayari ameshaamua kwa dhati kupigana katika vita ya kubana mianya inayotishia upotevu au matumizi mabaya yanayofanya na baadhi ya watu kutumia rasilimali za nchi vibaya kwa kujinufaisha wao huku taifa likiendelea kuwa masikini

Hii siyo vita ndogo, ni kubwa sana inayohitaji ujasiri na ari kubwa ya kujituma, hivyo ni lazima Watanzania wote tumuunge mkono ili asiyumbishwe na waliokuwa wanajinufaisha na rasilimali hizi", alisema Tumaini wakati wa mazoezi ya nyimbo hizo kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala, Dar es Salaam.
Mwanamuziki nguli Juma Abdallah 'Jerry' akikipapasa kinanda kwa mkoni mmoja kuonyesha umahiri wake, Kundi la TOT Plus lilipokuwa katika mazoezi ya nyimbo tatu, leo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala Dar es Salaam
Waimbaji Neca Twalib aliyechukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mwimbaji nguli na Mkurugenzi wa TOT Plus Marehemu Kampteni John Komba, akiimba na mwenzake Corobian Mkinga wakati wa mazoezi hayo
Mkurugenzi wa TOT Plus Gasper Tumaini (mwenye suti) akizungumza na baadhi ya wadau waliofika kushuhudia mazoezi hayo.
Mwimbaji nguli Hadija Kopa na wenzake wakiimba wakati wa mazoezi hayo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...