Kikundi cha Uzalendo Kwanza ikishirikiana na Kampuni ya Msama Auction Mart wameamua kuungana kwa pamoja katika kutokomeza kazi Feki za Wasanii hapa nchini.
Uzalendo Kwanza kupitia kwa Mwenyekiti wake, Steve Nyerere wameungana na Msama Auction Mart pamoja na kushukuru juhudi zinazofanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya yakukamata Walanguzi wa kazi hizo.
Steve Nyerere amesema wafanyabiashara katika Maduka Makubwa ya Filamu vifaa vya Soka wanafanya biashara hizo lakini hawalipi Kodi, hivyo wanawapongeza Msama Auction na TRA kuunga mkono jitihada zakutokomeza wizi huo.
"Wamejiajiri katika Taifa la Watanzania, wakipata faida kubwa, Kodi na Mapato makubwa yangepatikana", amesema Steve.Ameongeza kusema kuwa "Msama hatoshi, TRA peke yake hatoshi; Mhe. Rais hatoshi kama Wasanii wenyewe hatutounga mkono jitihada hizi".

Pichani kati ni Mwenyekiti wa kikundi cha Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini,kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart ,Alex Msama.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart ,Alex Msama akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi mapema leo,namna wanavyoshiriki zoezi la kukamata kazi feki za Wasanii,sambamba na wakwepa kodi kupitia kazi wasanii.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza,alipokuwa akizunguma nao mapema leo jijini Dar,
,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini.
,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini.
Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa filamu hapa nchin walipokuwa wakifuatilia mkutano huo mapema leo jijini Dar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...