Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura ameahidi kuunda kikosi kazi, kitakacho pita na kukusanya kiasi cha shilingi milioni 50 kwa Wadaiwa sugu wa Mamlaka ya maji safi Wilayani kibondo na kuhakikisha zinalipwa na kukabidhiwa kwa bodi mpya ya maji pamoja na kusitishia huduma ya maji kwa wale wote watakao shindwa kulipia madeni yao ya Nyuma.

Aidha Bura aliwaagiza wale wote wanao lima karibu na vyanzo vya maji kuacha kulima na kuondoa mazao yao kabla ya kuanza kutolewa kwa nguvu na kuharibiwa,vyanzo hivyo kujaa michanga wakati wa masika kutokana na baadhi ya wananchi kukosa uwelewa na kulima kwenye vyanzo na kupelekea upungufu wa maji katika wilaya hiyo.

Akizungumza jana Wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya maji Wilayani humo Mkuu huyo alisema, Serikali hadi sasa imeingia gharama ya kulipia deni la umeme ili kuhakikisha Wananchi wanaendelea kupata maji , wakati kuna baadhi ya Taasisi zikiwemo za Serikali na Wananchi wanadaiwa kiasi cha zaidi ya milioni 50.

Alisema Mamlaka hiyo imekuwa ikijiendesha kwa hasara hali iliyo walazimu kuanzisha mfumo mpya wa usambazaji wa maji kwa kutumia Sola ilikupunguza gharama za matumizi ya umeme ambayo hayaendani na Makusanyo ya mamlaka ya maji na kuagiza fedha hizo zitakazo kusanywa kuanzia kesho zipelekwe kwenye marekebisho ya sola na wananchi waweze kuepukana na kero ya ukosekanaji wa maji.

"Nimepitia orodha ya wadaiwa Mimi pia ni miongoni mwa wadaiwa nimekuta na mimi kuda deni kubwa halijalipwa, taasisi zote na Wananchi muhakikishe mnalipa deni hilo wananchi wamekuwa wakikosa maji kwakuwa uwezo wa mamlaka kulipia bili ya umeme haiwezi kutokana na madeni hayo kila mtu ataubeba msalaba wake nitahakikisha fedha hizo zinakusanywa ukishindwa kulipa utasitishiwa huduma", alisema Mkuu huyo.

 MKUU wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura alipokuwa akizungumza wakati wa kuzindua bodi mpya ya maji wilayani humo mkoani Kigoma
 Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakiwemo na watumishi wa bodi hiyo mpya ya maji wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...