Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India wamefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa wagonjwa 15 katika kambi maalum ya upasuaji ya siku sita inayomalizika kesho.
Upasuaji wa moyo unaofanyika katika kambi hii ambayo imeanza Jumatatu tarehe 8/11/2017 hadi Jumamosi tarehe 11/11/2017 ni ya upasuaji wa kufungua kifua kwa watu wazima. Upasuaji uliofanyika ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting), na kubadili milango miwili hadi mitatu ya moyo (Valve Replacement).
Kwa mara ya kwanza hapa nchini tumefanya upasuaji wa kurekebisa mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic Aneurysm Repair).
Tulifanya upasuaji kwa wagonjwa watatu kwa siku, wote hawa wanaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika. Baadhi yao ambao tumewafanyia upasuaji jana na juzi wako katika chumba cha uangalizi maalum na wengine wako wodini wameshaanza kufanya mazoezi.
Kama wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nje ya nchi Serikali ingelipia zaidi ya milioni 405 kwani gharama za mgonjwa mmoja kwenda kutibiwa nje ya nchi ni zaidi ya milioni 27. Gharama za matibabu haya hapa nchini kwa wagonjwa 15 ni milioni 225 (milioni 15 kwa mgonjwa mmoja).
Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri. Tunawashauri wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Moyo na Mishipa ya Damu ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji
kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na
waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji
ambayo imefanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India ambapo wagonjwa
15 wamefanyiwa upasuaji. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi Roberth
Mallya na kushoto ni Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi Anjela
Muhozya akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu
kutoka Hospitali ya Saifee Ali Ascar Beliranwalwa.

Mkutano
wa waandishi wa Habari ukiendelea kuhusu
kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na
Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini
India ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Upasuaji uliofanyika ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo
(CABG – Coronary Artery Bypass Grafting), kubadili milango miwili hadi mitatu
ya moyo (Valve Replacement) na
kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili
(Aortic Aneurysm Repair).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...