Kwa mara ya kwanza tangu Taasisi imeanza kutoa huduma ya matibabu ya upasuaji wa Moyo bila ya kufungua kifua tumefanya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono. Upasuaji tuliokuwa tunaufanya kwa wagonjwa wetu ni wa kutumia mishipa ya paja.Upasuaji wa moyo unaofanyika katika kambi hii ambayo imeanza Jumatano tarehe 15/11/2017 hadi Jumamosi tarehe 18/11/2017 ni ya upasuaji wa bila kufungua kifua kwa watu wazima. Upasuaji uliofanyika ni wa kuzibua mishipa ya moyo iliyoziba.

Aidha wageni nao wamepata muda wa kujifunza vitu vingi na kupata uzoefu mpya wa baadhi ya magonjwa na mambo ya kiteknolojia ambayo katika nchi yao hakuna.Tunaendelea kuwasisitiza wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati. Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri.
Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapougua na kuhitaji kupata matibabu. Kwa namna ya kipekee tunaishukuru sana Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) kwa kutuma wataalam wake wa magonjwa ya moyo kuja hapa nchini kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wetu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
18/11/2017
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...