Na Dotto Mwaibale, Chato
WAKULIMA
Wilaya Chato mkoani Geita wamefurahia mbegu bora ya mihogo, mahindi na
viazi lishe waliopewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) ili kuanzisha mashamba darasa ya mbegu hizo na kuzisambaza kwa
wakulima wengine katika maeneo mengine.
Wakizungumza
wilayani hapa leo kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa mashamba
darasa ya mbegu hizo katika vijiji vya Kibehe, Ipandikilo, Kitongoji cha
Kaseni, Kijiji cha Itale na Bukiliguru kilichopo Kata ya Bwanga
walisema mbegu hizo walizokabidhiwa na COSTECH kwa kushirikiana na
Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo ni mkombozi kwao.
Ofisa
Kilimo wa Kata ya Kachwamba, Hamisi Matesi alisema Costech
kuwapelekea wakulima mbegu hizo itawasaidia sana kupata chakula wananchi
wa kata hiyo ziada watauza.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis akizungumza kwa niaba
ya wananchi wa kijiji hicho alisema wakulima walikuwa wakipata mavuno
machache ya mahindi na mihogo kwa kuwa hawakuwa na mbegu bora hivyo
baada ya kufunguliwa kwa shamba darasa la mbegu hizo katika maeneo yao
wanategemea kupata mazao mengi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari aliwataka
wananchi hao kutambua kuwa mpango huo wa serikali ya awamu ya tano
unawategemea sana wakulima katika kilimo hivyo fursa hiyo walioipata ya
kupelekewa mbegu hizo wasiipoteze.
“Hakikisheni
mbegu hizi bora za mihogo mnazopewa mnazitunza ili kutoa nafasi kwa
wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu bora za kilimo hiki kupitia shamba
darasa hili ili kila mkazi wa Chato aweze kulima na kuzalisha kwa tija”
alisema Mhandisi Hari.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi (kushoto), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akimkabidhi mbegu ya viazi lishe kwa ajili ya shamba darasa la Kijiji cha Kibehe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani Chato leo.
Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiandaa shamba lao la mbegu.
Wanakikundi cha Umoja cha Kijiji cha Kibehe kilichopo Kata ya Kigongo wakiwa kwenye uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe na mihogo.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi wa Wilaya ya Chato, Monica Mulongo akizungumzia vitamini A inayopatikana kwenye viazi lishe ambayo ni muhimu kwa watoto.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...