Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wameendele kujadili jinsia ya kutekeleza kampeni ya Wizara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ya jamii na mbinu mahususi katika kufanikisha utekelezaji wa programu mbalimbali zinazohusiana na maendeleo jumuishi ya jamii zetu. 

Mbinu hii ina wawezesha wataalam wa maendeleo ya jamii katika sekta za umma na sekta binafsi kuhusisha wananchi kubainisha rasilimali na uwezo wa kitaalamu katika kuanzisha miradi ya kimaendeleo na kiuchumi ambayo inalenga kukuza ustawi wa watu wenyewe.

Mpango wa kuamsha ari ya kushiriki kazi za maendeleo ya Taifa unahitaji umuhimu mkubwa wa takwimu katika kupima matokeo ya utekelezaji wa miradi na uwekezaji kuanzia ngazi ya Kata mpaka taifa.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitoa mada kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuhusu kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo yao katika Mkutano Kazi wa mwaka unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akiwasilisha mada ya Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa Mkutano Kazi wa Mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akiwasilisha mada ya kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake nchini wakati wa Mkutano Kazi wa Mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya zote nchini wakifuatilia mijadala ya kuhuisha ari ya wananchi kuitikia kazi za maendeleo yao na kujenga uelewa kuhusu agenda ya kushiriki katika kufikia uchumi wa kati na wa viwanda wakati wa Mkutano wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya jamii unaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...