Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo amewataka watendaji wa Manispaa ya Temeke kutoa ushirikiano ili kuwezesha kukamilika kwa mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) na watendaji watakaoshindwa kutoa ushirikiano huo watashughulikiwa.
Akizungumza leo wakati uzinduzi wa jengo la ofisi na Maabara za mradi  wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) lililojengwa katika Manispaa ya Temeke, Jaffo amesema mradi huo utawezesha manispaa ya Temeke kuwa ya sura mpya na kuwa mfano kwa jiji la Dar es Salaam.
Amesema mradi utawezesha kujengwa kwa barabara na mifereji na hivyo kupunguza msongamano wa magari.
Amesema mradi huo ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) utatekelezwa katika jiji zima la Dar es Salaam katika kupanga mji kuwa na makazi bora yenye huduma zinazoendana na makazi hayo.
“Temeke mmekuwa na  bahati ya kuwa ya kwanza kutekeleza mradi huu, shirikianeni kuifanya Temeke kuwa ya kisasa kwa kuondoa Temeke  iliyokuwepo zamani isiyokuwa na miundombinu rafiki kwa makazi ya wananchi,” amesema.
Mratibu wa mradi huo katika manispaa ya Temeke, Edward Simon amesema Shilingi bilioni 265 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi barabara na mifereji. Amesema jumla ya kilometa 91 za barabara za ndani zitajengwa kwenye manispaa hiyo.
Amesema mradi huo ukikamilika utawezesha barabara kupitika na kupunguza mafuriko kutokana na kutengenezwa mifereji.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akizungumza na katika uzinduzi wa jengo la ofisi na Maabara za mradi  wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akikabidhiwa  mfano ufunguo wa jengo la mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP)  kutoka kwa Mratibu wa Miradi, Devis Shemangali unaofadhiliwa  na Banki ya Dunia  leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...