Na Karama Kenyuko-Globu ya Jamii.

Watu 10 (pichani). wanaosadikiwa kuwa wachezaji wa Judo nchini, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 13, likiwamo la kusafirisha binadamu kwa njia haramu, kughushi na kutoa taarifa za uongo katika Ubalozi wa Italia nchini Tanzania.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na Pamela Shinyambala na Mwanaamina Kombakono.

Washtakiwa hao walitajwa kuwa ni, Kashinde Bundala, Said Ally, Mafunda Ali, Abdulrazak Baus, Mwamba Mungia, Hafidhi Said, Abubakari Nzige, Athumani Ngondo, Endrew Mlugu na Ahmed Magogo.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi, Godfrey Mwambapa imedaiwa kati ya Oktoba Mosi na Novemba 3/2017 jijini Dar es Salaam mshtakiwa Bundala 

chini ya kisingizio cha kuhudhuria mashindano ya Sankuku Judo na mafunzo aliajiri na kuwasafirisha watu tisa, Kwenda Milan nchini Italia kwa ajili ya kufanya kazi kwa nguvu.

Watu hao ni, Ally, Ali, Baus,Mungia Said, Nzige, Nyondo Mlugu na Magogo.

Katuga amedai Oktoba 5/ 2017 huko Mwananyamala, mshtakiwa Bundala alighushi barua ya Oktoba 5,2017 akionyesha kuwa Umoja Judo Klabu umeomba ushiriki wa timu ya Judo ya Tanzania katika mashindano ya 28 ya Sankuku Judo wakati akijua si kweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...