Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 07/11/2017 huko maeneo ya Tegeta IPTL lilifanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T. 897 ARF aina ya FUSSO likiwa limebeba nyaya za umeme Roller/Drum 05 zikiwa ndani ya gari hilo.

Aidha dereva wa gari hilo aliwaelekeza askari watuhumiwa wenzake na baada ya upekuzi zilikamatwa Roller/drum 02, mashine ya kupaka, rangi na makopo Mmatatu (3)matupu ya rangi yaliyotumika kubadilisha uhalisia wa Roller/drum, zote zilikutwa kwa mtu aitwaye ZAWAKO KASIBA na mke wake, mkazi wa IPTL Tegeta na watuhumiwa wengine wanne.

Watuhumiwa wote wamekamatwa na mawasiliano yalifanyika na Shirika la umeme (TANESCO) na walifika kuzitambua nyaya hizo na kugundua kuwa ni mali za Shirika ambazo ni DRUM 07 zikiwa na mita 21,000 zenye thamani ya Tsh Milioni 70.7

Jumla ya watuhumiwa sita wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo akiwemo mwanamke mmoja.

Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaotuhumiwa kuhujumu miundo mbinu ya TANESCO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...