Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati wamempokea rasmi Katibu Mkuu mpya,
Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.
Mapokezi hayo yalifanyika Oktoba 31, 2017 na kuongozwa na Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda.
Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali wakati wa mapokezi hayo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu
mpya wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), mara baada ya
Katibu Mkuu kuwasili rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kulia),
akimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda
(kushoto), mara baada ya kuwasili rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini
Dodoma.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua
(kushoto), akisalimiana na wafanyakazi mbalimbali wa Wizara (kulia),
alipowasili rasmi Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...