Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Bi. Suzan Mlawi, amepongeza utendaji kazi na ubunifu unaofanywa na Idara ya Habari- MAELEZO katika kuuhabarisha umma juu ya masuala mbalimbali yanayofanywa na serikali ya Awamu ya Tano.

Pongezi hizo amezitoa leo wakati alipokutana na uongozi wa Idara ya Habari- MAELEZO katika kikao kazi kilichokifanya mahsusi kufahamu majukumu na changamoto zinazoikabili idara hiyo.

“Nyinyi ni idara muhimu sana na yenye majukumu makubwa sana ya kuisemea na kuitetea serikali hivyo mna jukumu la kufanya kazi kwa weledi, kwa kufuata Sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma pamoja na taaluma na miiko ya uandishi wa habari ili muwe mfano kwa wanatasnia ya habari mnaowasimamia” alisema Bi. Mlawi.

Aliitaka Idara ya Habari kuhakikisha wanakuwa na vikao vya mara kwa mara na vyombo vya habari ili kushauriana namna nzuri ya kuendeleza tasnia ya habari lakini pia kukumbushana majukumu na wajibu wao kama wanahabari hasa katika kuzisukuma mbele ajenda mahsusi za serikali ya Awamu ya Tano, kama kujenga Tanzania ya viwanda, kudumisha uzalendo na mapenzi kwa nchi pamoja na kusisitiza umuhimu wa wananchi kulipa kodi kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Bi. Mlawi ambaye alifuatana na Naibu Katibu wake Bw. Nicolaus Wilium, alisisitiza umuhimu wa idara kuendeleza ubunifu katika mawasiliano yake na umma ili kuwawezesha wananchi wakiwemo wa vijijini kuwa na ufahamu mzuri wa mambo mengi makubwa na mazuri ambayo serikali imefanya.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (kulia) nakala ya Jarida la Nchi Yetu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu huyo kutembelea Ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Willium (kulia) nakala ya Jarida la Nchi Yetu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Susan Mlawi katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Idara hiyo kujionea utendaji kazi wake mapema leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nicholaus Willium.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...