Antu
Mandoza akiwa katika picha ya pamoja na Muigizaji nyota wa Filamu
kutoka nchini Nigeria Ramsey Noah wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwigizaji
nyota wa filamu na Mkongwe wa tasnia hiyo kutoka nchini Nigeria ,Ramsey
Noah ametamani kufanya kazi na nyota mwingine wa movie anaechipukia kwa
kasi katika tasnia hiyo hapa nchini,ambae ameng'ara vilivyo katika
filamu ya 'KIUMENI' , Antu Mandoza wa Tanzania .
"Anaonekana
ni binti mweye kipaji,anaejiamini,kwa hakika natamani nipate muda wa
kubaini kipaji chake zaidi kwa kufanya nae angalau hata filamu
moja,itaweza kumsaidia zaidi kujitanua na kutambulika Kimataifa",alisema
Ramsey huku akimtazama Antu kwa tabasamu laini la ucheshi.
Antu
Mandoza ni Binti wa makamo hivi,lakini amejaaliwa kuwa na kipaji cha
uigiza wa filamu na mwenye uthubutu wa kufanya jambo.Antu Mandoza na Ramsey Noah
walikutana katika Warsha fupi iliyoandaliwa na Sahara Group
iliyofanyika hotel ya Hyatt Dar Es Salaam mnamo Desemba 16 2016,ambayo
pia iliwahusisha wasanii mbali mbali wa bongo movie .
Ikiwa
ni movie yake ya kwanza 'KIUMENI', Antu Mandoza amefunguka na kusema
kuwa mwaka ujao utakua ni mwaka wa kazi tu, kama ilivyo Slogan ya Raisi
Dkt John Pombe Magufuli,na anategemea kufanya kazi na Ramsey Noah na
wasanii wengine wengi wa Ndani na Nje ya Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...