NA K-VIS BLOG, FELIX ANDREW 
WAAJIRI Tanzania Bara wametakiwa kuwashirikisha wafanyakazi wao kabla ya kufanya maamuzi mbali mbali ili kuendelea kudumisha amani na mshikamano maeneo ya kazi.

Ushauri huo ulitolewa jjini Dar es Salaam jana na Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde, wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC)

Alisema kuwa uongozi shirikishi na wa pamoja ndiyo njia pekee itakayopunguza migogoro maeneo ya kazi, hivyo waajiri hawana budi kuhakikisha jambo hilo linazingatiwa ipasavyo.
“Lengo kuu la uongozi shirikishi na wa pamoja ni kujadiliana changamoto mbali mbali na kuzitatua kwa nia ya kufikia malengo,” alisema.

Mavunde aliwaasa wafanyakazi nchini kuondokana na urasimu katika kutoa huduma mbali mbali kwa jamii.
“Urasimu katika utoaji wa huduma ni changamoto kubwa sana ambayo inaisumbua nchi naomba sana msifanye hivyo kwa manufaa ya taifa letu,” alisema.
Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (wakwanza toka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (wa pili toka kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza za Wafanyakazi mapema leo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (kulia) wakionyesha
Wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC) wakifurahia uzinduzi huo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...