Waziri wa Maji na umwagiliaji Mh. Mhandisi Isack Kamwelwe, amewahakikishia wananchi wa kata ya Mtwango halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kuwa, mradi mkubwa wa Maji wa Sawala wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja, utaanza kujengwa mapema mwezi januari mwakani mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kutiliana saini na mkandarasi mteule.

Waziri huyo mwenye dhamana ya Maji nchini, ametanabaisha hilo wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mufindi, iliyokuwa na lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa Wilayani humo.

Waziri Kamwelwe, amesema baada ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kukamilisha taratibu zote za manunuzi na kumpata Mkandarasi atakaye tekeleza mradi huo, Ofisi yake inakamilisha uhakiki wa mkataba na ifikapo mwezi wa kwanza mwaka 2018, itatoa kibali kwa Ofisi ya Mkurugenzi ili aendelee na hatua ya mwisho ya kusaini kandarasi hiyo yenye jumla ya shilingi bilioni (1.8).

Mradi wa Maji wa Sawala unatarajiwa kujengwa na kukamilika kwa muda wa kipindi cha miezi (12) huku wakazi wa Vijiji vinne vya Mtwango, Kibao, Sawala na Lufuna ndio watakao nufaika na mradi huu, ikiwa ni utekelezaji wa shabaha ya Serikali inayokusudia kutatua kero ya Maji kwa asiliamia (85) kwa wakazi wa Vjijini ifikapo mwaka 2020.
Waziri wa Maji na umwagiliaji Mh. Isack Kamwelwe, akizungumza na Viongozi wa Wilaya ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi ya Maji.
Waziri wa Maji na umwagiliaji katikati akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William kusho pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe kulia, mara baada ya kuwasili Wilayani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...