Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa pili kulia), Mganga Mkuu wa Serikali, Mohamed Kambi Bakari ( kulia) wakisaini hati ya mkataba maalumu wa utendaji kazi (Performance Contract) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ( kulia). Wengine wanao shuhudia tukio hilo ni Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daud Msasi na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Ilangwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akimkabidhi hata hizo za mkataba Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akikata utepe kuashiria uzinduzi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akihutubia kwenye uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD)imezindua Mpango Mkakati wa Kati 2017 – 2020 ili kuongeza kasi ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini. 

Akizindua mpango mkakati huo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya ameipongeza MSD kwa kuandaa upya mpango huo ambao wamejikosoa na kuboresha maeneo muhimu ili kuendana na vipaumbele vya serikali na mahitaji ya wananchi wa Tanzania, hususan vituo vya Afya vya Umma.

Maeneo hayo muhimu ni pamoja na Kujitegemea kifedha, kuuhuisha Mnyororo wa Ugavi, Kuboresha mfumo wa Tehama, Matumizi yenye tija ya Rasilimali Watu, Utawala na Ushirikishwaji wadau.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya ameingia mkataba maalumu wa utendaji kazi (Performance Contract)na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu ili kuhakikisha utekelezwaji wa haraka wa Mpango mkakati uliozinduliwa.

Aidha katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema atahakikisha Mpango Mkakati 2017-2020 unatekelezwa ambapo kila Mkurugenzi na Mameneja wa MSD wameingia mikataba inayopimika ya utendaji kazi. 

Bwanakunu aliongeza kuwa ufuatiliaji wa utendaji utafanywa kupitia Ofisi maalumu ya kusimamia utekelezaji wa mikakati ya MSD(Strategic Management Office)Tayari kila Mkurugenzi na mameneja wa MSD wamesaini mkataba kutekeleza Mpango Mkakati huo wa Kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...