MKUU wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo,Mbunge wa Jimbo hilo,Balozi Adadi Rajab na wakazi wa wilaya hiyo wakishirikiana kwa pamoja wameanza kuchimba msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika Kijiji cha Lusanga Kata ya Lusanga ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya kutokuwepo kwa kipindi cha miaka 37.

Hatua ya viongozi hao ina lengo la kuandika historia tokea wilaya hiyo ilipoanzishwa mwaka 1974 ambapo wananchi walikuwa wakitegemea kupata huduma za matibabu kwenye hospitali ya Teule Muheza kutoka maeneo mbalimbali kabla ya kufikiria kuanzishwa kwa hospitali hiyo ambayo itakayogharimu zaidi ya bilioni 11.

Akizungumza wakati akishiriki zoezi la uchimbaji wa mtaro wa Hospitali hiyo na kupokea mifuko ya saruji 600 ya Lucky kutoka kwa Kampuni ya kuzalisha Saruji ya Kisarawe, Mhandisi Mwanasha alisema waliamua kufanya hivyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya huduma ya afya ambayo ilimlazimu wakati ameteuliwa kuiongozi wilaya hiyo kukutana na wadau kuweza kuona namna ya kuweka mikakati ya kupatikana kwake.

Aidha kutokana na kuwepo kwa hospitali ya wilaya walikuwa wakilazimika kutimia hospitali ya teule Muheza tokea ilipoanzishwa lakini imeonekana kuzidiwa na watu wanaohitaji huduma hasa ukizingatia pia zahanati na vituo vya afya vipo vichache huku wananchi wakiongezeka.

“Nilibaini changamoto ya hospitali ya wilaya wakati nilipokuwa nikifanya vikao kwa kuzunguka kata zote nikaona tatizo la huduma ya afya ni kubwa sana na hivyo kuonekana kuna haja ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza lakini hata kwenye baraza la madiwani suala hilo lilizungumzwa”Alisema
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani humo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Like Gugu wakishuhudia tukio hilo.
Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akichimba mtaro kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo eneo la Lusanga wilayani humo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo,Like Gugu
Sehemu ya wananchi wakishiriki katika uchumbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...