WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameagiza
taasisi zote zinazohusika na udhibiti wa maudhui ya luninga nchini
kubuni mkakati wa pamoja wa kuboresha udhibiti.
Dk Mwakyembe ametoa rai hiyo baada ya kuzikutanisha taasisi hizo za udhibiti leo jijini Dar Es Salaam.
"Nyinyi
nyote ni taasisi za Serikali, hivyo tengenezeni mkakati wa kufanya kazi
kwa pamoja kudhibiti maudhui mabovu ili kulinda maadili ya jamii
yetu," alisema.Waziri Mwakyembe alifanya mkutano
wa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya Filamu
Tanzania (TFB) na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)."Kuna
hitaji za kuongeza uwezo wa kufuatilia maudhui ya luninga ikiwa ni
pamoja na filamu zote ili kubaini maudhui hasi kwa jamii yetu na
kuzishughulikia ipasavyo kabla hazijaleta madhara kwa jamii," alisema.
Alisema
changamoto za ongezeko la mahitaji ya jamii zinazidi kukua kwa haraka
kutokana na kasi ya maendeleo hivyo ni vizuri kuhakikisha kuwa majawabu
yake yanapatikana.Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Susan
Mlawi, alisema Wizara itaangalia jinsi ya kuunganisha majukumu ya
taasisi zinazosimamia maudhui ya vyombo vya utangazaji nchini ili
kuimarisha udhibiti wa pamoja.
Akiongea
katika mkutano wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dodoma
mapema wiki hii, Rais John Pombe Magufuli aliiagiza Wizara ya Habari na
TCRA kutosita kuvichukulia hatua vyombo vya utangazaji zinavyokiuka
kanuni za utangazaji nchini.
Dk Mwakyembe akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA,Bi.Valerie Msoka,
Kulia
ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Suzan
Mlawi, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Eng James Kilaba na Mkurugenzi wa
Utangazaji wa TCRA, Chief Fredrick Ntobi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...