Na Mathias Canal, Morogoro

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa leo Disemba 29, 2017 amewaagiza wafanyabiashara wa mbolea kote nchini walioweka mgomo wa kupeleka mbolea kwa wakulima kufikia 30 Disemba 2017 wawe wamefungua maghala yao kwa ajili ya kuwauzia mbolea wakulima.

Alisema endapo wafanyabiashara hao wasipofanya hivyo serikali itawanyang'anya leseni zao haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wafanyabiashara wenye uwezo wa kufanya jukumu hilo pasina kuwaumiza wakulima kutokana na bei ghali ya mbolea.

Mhe Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) Mara Baada ya kubaini kuwa kuna wafanyabiashara ambao wameanza kufunga maghala kwa madai ya kupanda kwa mbolea katika soko la Dunia.

Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kuijaribu serikali kwani malalamiko yao ya kupanda kwa bei katika soko la Dunia hayana tija kwani mbolea zote zilipo nchini tayari wakishanunua kipindi soko likiwa kwenye unafuu mkubwa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akikagua mbegu zilizohifadhiwa ghalani kabla ya kuanza kusambazwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge (Kulia) na Meneja uzalishaji Wakala wa Mbegu Ndg Charles Levi (Kushoto). Picha Zote Na Mathias Canal 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo baada ya kukagua baadhi ya mashine za mbegu alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna mbegu za mazao mbalimbali zilivyohifadhiwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...