Wapendwa wadau wa Libeneke la Globu ya Jamii, ni matumaini yetu kuwa mu wazima kabisa na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku katika kuisaha noti (japo wengine hulalamika kuwa vyuma vimekaza) ili kuendelea kusongesha maisha yetu ya kila siku. kwa kweli niwapongeze sana nyote. 

Leo tupo kwa sikukuu ya Krismas ambayo ni moja ya sikukuu za mwisho wa mwaka huku tukielekea kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, tunapaswa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi pamoja na vyote vilivyomo ndani yake kwa kutujaalia afya njema katika kipindi kizima cha mwaka 2017 na tuzidi kumuomba kwa kila hali ili aweze kutujaalia zaidi na zaidi katika kipindi kijacho cha mwaka 2018 na kuendelea, kwani yeye ndiye muweza wa yoote.

Wadau wetu Wapendwa, kwa namna ya kipekee kabisa napenda kuchukua fulsa hii kutoa salamu zetu za dhati kwenu ikiwa ni kwa niaba ya timu nzima ya Globu ya Jamii na mitandao yake mingene, katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismas na kuwa maandalizi mema ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2018 ambao siku chache tu zijazo tutakuwa tumeshaufikia kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu.

Hivyo basi kama kuna tuliyokoseana katika kipindi kilichopita basi yapaswa tusameheane kwani hayo yaweza kuwa ni mapungufu ya kibinadamu na kusameheana kwetu ndio muendelezo mzuri wa maisha yetu na Libeneke kwa ujumla na kwa yale mema tuliyoyafanya kwa kipindi hicho basi tusiyaache na tuyaendeleze zaidi na zaidi.

Wadau wapendwa naomba kuwaasa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kuwa watulivu kabisa katika kusherehekea kwetu kwani ni mambo mengi huwa yanatokea katika rokipindi hiki, hivyo basi yatupasa tusherehekee kwa amani na utulivu sherehe zetu hizi.

kwa haya machache naomba niwatakie sikukuu njema ya Krismas na makaribisho mema ya mwaka mpya wa 2018 wadau wetu wote popote pale walipo, bila kusahau Globu ya Jamii inatoa kwenu wadau kuweza kutuma salamu zenu za sikukuu kwa yeyote umpendaye, na salamu hizo zitumwe kwa email hizi

issamichuzi@gmail.com 
au
othmanmichuzi@gmail.com

zikitufikia nasi tutaziweka ukurasani kama ilivyo kawaida yetu siku zote.

Ahsanteni sana na Sikukuu njema.

- Ankal

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ASANTE SANA ANKALI KWA KUTU HABARISHA.
    HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...