DODOMA: Shirika la LEAD Foundation linalojihusisha na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu utunzaji wa mazingira limezindua mradi wa Kisiki Hai Mkoa wa Dodoma wenye lengo la kukomboa ardhi iliyochakaa ya mashamba na malisho ili kupambana na baa la njaa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira wakati wa ufunguzi wa mradi huo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la LEAD Foundation, Mhandisi Njamasi Chiwanga amesema kuwa lengo la Mradi wa Kisiki Hai ni kuhakikisha wanafikia jumla ya kaya laki moja na themanini (180,000) ambazo zipo katika hali mbaya ya mazingira ziweze kutunza hekta 180,000 kwa kustawisha miti milioni 14 kwa njia ya Kisiki Hai (FMNR - Farmer Managed Natural Regeneration) ifikapo mwaka 2020.

Njamasi amesema kuwa mikakati waliyonayo katika mradi huo ni pamoja na kujenga mshikamano wa wadau wote wa mazingira hususan viongozi wa wilaya, wakuu wa idara na taasisi mbalimbali, madiwani, watendaji wa kata pamoja na viongozi wa dini ili kuweza kushirikiana katika kufanikisha kukomboa mazigira. Kwa kuanzia mradi unatarajia kunufaisha tarafa mbili zilizo athiriwa zaidi na uharibifu wa mazingira katika kila wilaya ili kufikia nusu ya kaya zote za Mkoa wa Dodoma.

Mgeni Rasmi katika ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Deo Ndejembi amesema anaunga mkono mradi huo na atahakikisha unafanikiwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mambo mbalimbali watakayo hitaji katika kufanikisha mradi huo.Kwa upande wao baadhi ya wadau waliofika katika ufunguzi wa mradi huo wamesema kuwa mpango wa Kisiki Hai ni mzuri na wana hakika iwapo wananchi wataupokea vizuri baada ya muda mfupi changamoto ya uharibifu wa mazingira katika Wilaya ya Kongwa itakuwa ni historia.

Kisiki Hai ni mradi wa miaka mitatu na unatarajiwa kufikia Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na kwa sasa umenza katika Wilaya ya Kongwa ambapo umeanza na tarafa ya Kongwa na Mlali za wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi akifungua rasmi mradi wa LEAD Foundation.

 Mkurugenzi wa Programu - LEAD Foundation Mhandisi Njamasi Chiwanga akiwasilisha mpango wa Programu
Wadau walio hudhuria warsha ya mazingira ya Kisiki Hai

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...