Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (wa pili kulia) na wajumbe wengine wa kamati hiyo wakimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (wa kwanza kushoto) kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea.
Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour (katikati) akisaini kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli kabla ya kumkabidhi Balozi Augustino Maiga.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo na Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina alipokutana nayo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour

Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...