KAMATI maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina imekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa mazungumzo maalum walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waziri Dk. Mwakyembe, Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck alisema michezo inaumuhimu mkubwa kwa jamii kwani ni kiungo kinachotumika kujenga mshikamano na kudumisha amani kwa mataifa mbalimbali na jamii kwa ujumla.

Aliwahimiza wanahabari nchini kuendelea kuandika habari za Palestina kiusahihi ili kuielimisha jamii juu ya suala hilo na pia kupaza sauti na hatimaye suluhu kupatikana eneo hilo, aliwataka vijana kupenda kusoma historia za maeneo anuai ikiwemo mvutano kati ya Palestina na Israeli kwa ajili ya kujijengea uelewa wa mambo duniani.

Kwa upande wake Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour akizungumza na waziri alitoa ombi la mechi ya kirafiki kimataifa kati ya Tanzania na Palestina kudumisha zaidi uhusiano uliopo pande mbili. Kamati hiyo ilipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu katika mdahalo, asasi za kiraia na Jukwaa la Wahariri.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akikabidhiwa kitabu cha picha na historia ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli alipotembelewa na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisalimiana na Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour (wa pili kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...