Katibu
Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu Nyakia Ally Chirukile akichangia damu
baada ya kushiriki zoezi la Usafi wa kila jumamosi ya mwisho wa
Mwezi,zoezi ambalo lilikwenda sambamba na upandaji wa miti zaidi ya 2000
pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka Kilema.
Akizungumza
baada ya shughuli nzima,Ndugu Nyakia aliwaomba wananchi wa wilaya ya
Chemba na mkoa wa Dodoma kwa ujumla,kuunga mkono juhudi za Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassani katika
suala zima la uhamasishaji wa kupanda miti na kuhakikisha mkoa huo
unakuwa wa kijani .
Baada
ya kufanyika shughuli ya uchangiaji Damu,pia kulifanyika tukio la usafi
na upandaji wa miti zaidi ya 2000
pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka
Kilema,kuhakikisha mkoa wa Dodoma unakuwa wa kijani,kufuatia kampeni
maalum ya upandaji miti iliozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa
Rais,Mama Samia Suluhu Hassan mkoani humo na kushirikisha viongozi
mbalimbali wa Kitaifa na Wadau wengine wa Mazingira.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu Nyakia Ally Chirukile akishiriki
shughuli ya upandaji wa miti zaidi ya 2000
pembezoni mwa barabara ya Dodoma -Babati kuanzia Kidoka mpaka
Kilema,baada ya zoezi hio Ndugu Nyakia pia alishiriki tukio la Usafi na
uchangiaji wa Damu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...