Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Kishapu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza halmashauri za wilaya nchini kuhakikisha zinasimamia kikamilifu kilimo cha zao la pamba ili kiwe na tija.
Ametoa agizo hilo katika kikao na wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga ambapo alizitaka halmashauri hizo kuratibu shughuli za kilimo hicho kwa kuwapangia ratiba maafisa ugani kuwatembelea wakulima kuwapa elimu.
Akizungumza katika kikao hicho kilichoikutanisha mikoa zaidi ya 10 inayolima pamba aliwataka watendaji wakuu wa halmashauri hizo kuhakikisha kila kata na kijiji kunawepo na maafisa ugani ili wasimamie kikamilifu kilimo.
Majaliwa aliwataka maafisa ugani waliopo katika halmashauri hizo kuwafikia wakulima mashambani ili kuwapa elimu na kutatua changamoto zinazowakabili kuhusu kilimo hususan cha pamba.“Tunataka kuhahakikisha pamba inaleta heshima na inaongeza mapato ya mkulima mmoja mmoja na hata taasisi zetu yaani halmashauri na mikoa zinaingiza mapato kupitia zao la pamba hivyo kila mmoja awajibike,” alisisitiza.
Pia, aliagiza pia ziweke mpango kazi wa namna ya kukiletea mafanikio kilimo hicho huku akisisi kuwa na kwamba atafanya ziara kukagua akisema atataka apewe taarifa ya maendeleo ya kilimo hicho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao na wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga. Wengine picha ni kuanzia kushoto ni Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba.
Sehemu ya wakuu wa mikoa inayolima zao pamba wakifuatilia matukio katika kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati mwenye miwani) akifurahia wimbo na viongozi wengine mara baada ya kuwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho. Wengine pichani kuanzia kushoto ni Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Wakuu wa wilaya za Shinyanga ambazo ndizo miongoni mwa wakulima wa pamba, kuanzia kushoto ni Fadhil Nkurlu (Kahama), Nyabaganga Taraba (Kishapu) na Josephine Matiro (Shinyanga) na kulia pichani Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi wakifuatilia matukio.
Sehemu ya wakuu wa mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Shinyanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...