NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Kidatu.
MATENGENEZO
makubwa ya mashine namba moja kati ya nne za kufua umeme wa maji kwenye Kituo
cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro yamefikia zaidi ya asilimia 95
kukamilika.
Msimamizi wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda amewaambia wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kituo hicho Desemba 22, 2017.
"Kwa sasa tumeanza majaribio ya mashine kuzunguka bila kutumia nguvu za maji, mafundi wanazungusha mashine hiyo kwa kutumia mikono ili kuangalia usahihi wa unyookaji wa shafti,”alisema.
Alisema hatua itakayofuata ni kuunganisha kipande yanapoingilia maji ili kuzungusha huo mtambo na sehemu ya kuzalishia umeme na Jumapili mafundi hao wanaoshirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia wataanza majaribio ya kuzungusha mtambo wenyewe.
Aidha Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi Amesema Kidatu kuna mitambo minne na kila mmoja unauwezo wa kuzalisha umeme Megawati 51 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 204 za umeme ambao unaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
”Tuliona tufanye matengenezo makubwa kwani kila baada ya miaka 20 huwa tunafanya zoezi kama hili ili kurejesha mashine kufanya kazi bora kwa kipindi hicho ili kuhakikisha mtambo unarejea kwenye hali yake ya kawaida.” Alisema.

Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), wakishirikiana na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia, wakifanya matengenezo makubwa ya mashine namba moja ya kufua umeme, kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro Desemba 22, 2017. Kituo hicho kina jumla ya mashine 4 (Turbines) za kufua umeme wa Megawati 204.
Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine turbines kwenye bwawa la Kidatu mkoani Morogoro. |
Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.

Wasimamizi wa chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini wakati walipotembelewa na wahariri wa vyombo vya habari Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...