Mkuu wa Mkoa wa Rukwa , Wangambo akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mapazia na Mashine Dinious Swai juu ya bidhaa za ngozi zinazozalishwa na kampuni ya Woiso katika maonesho ya viwanda katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Petro Limu juu ya mashine ya kulimia yenye gharama nafuu wakati alipotembelea banda la chuo kikuu cha Dar es Salaam katika maonesho ya viwanda katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza na mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mathias Halinga baada ya kupata maelezo mbalimbali juu ushiriki maonesho ya viwanda yanayofanyika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza katika Banda la Mamlaka ya Elimu na Ufundi, Stadi (VETA) wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya viwanda yanayofanyika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari na Elimu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Sigifrid Mfey akizungumza na mwananchi juu ya madhara ya vipodozi bandia wakati mwananchi huo alipotembelea banda la TFDA katika maonesho ya viwanda yanayofanyika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Pendo Gondwe akizungumza na mwananchi juu ya ya uwekezaji unaavyotakiwa kufuata taratibuyoa wakati mwananchi huyo alipotembelea banda TIC katika maonesho ya viwanda yanayofanyika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...