Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya Utunzaji bora wa Mahesabu na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA), baada ya kufanya Vizuri kwenye kada hiyo katika Mwaka wa fedha 2016/2017.
Akipokea tuzo hiyo Afisa mkuu wa Masuala ya fedha wa TANESCO, Bi RENATA NDEGE ameishukuru Bodi ya Wahasibu na wakaguzi (NBAA), kwa kutambua Utendaji Kazi wa Shirika hilo la Ugavi wa umeme hapa Nchini.
" Napenda kuishukuru Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi kwa kuonesha imani katika Utendaji kazi wetu hususani kwenye Kada hii ya Masuala ya Utunzaji wa fedha, Sisi kama Idara tunaahidi Kuimarisha Utendaji Kazi wa TANESCO kwa Kushirikiana na NBAA" alisema Bi RENATA.
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Fedha katika Shirika la Umeme (TANESCO), wakionekana kufurahia tuzo waliyokabidhiwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu, wameuambia Mtandao wa www.habari360.co.tz kwamba Wataendelea Kuchapa kazi Kwa weledi ili Kulisaidia Shirika Kutimiza Majukumu yake kwa Umma wa Watanzania.
Tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa Idara ya Fedha ya Shirika la Umeme (TANESCO), imeakisi Ubora wa Shirika hilo la Umma katika Utunzaji wa Mahesabu ya Fedha.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...