Miss Universe Tanzania, Lilian Erica Maraure  amelalamikia hatua ya majaji ya kutomuingiza hata katika hatua ya16 bora ya fainali hizo richa ya kuongoza katika kura za mitandao.

Lilian ambaye ni mtangazaji wa TBC international, alisema hayo mara alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere alisema kuwa miaka yote, warembo wanaongoza katika kura za mitandao upata nafasi ya kuingia katika hatua ya fainali tofauti na mwaka wake.

Alisema kuwa ameshangazwa hatua ya majaji ya kuwaingiza katika hatua ya 16 bora warembo ambao kuwenye kura za mitandao hawafanya vizuri na kumuacha wewe.

“Natambua kuwa maamuzi ya majaji ni ya mwisho, lakini nahoji hatua iliyochukuliwa ya kuacha kuingia hatua ya 16 bora na hata kwenye fainali pamoja na kupigiwa kura nyingi sana na kuongoza,” alisema Lilian.

Katika mashindano hayo, Mrembo wa Afrika Kusini, Demi-Leigh Nel-Peters alitwaa taji hilo. Pamoja na matokeo hayo,Lilian alisema kuwa amepata uzoefu wa kutosha mbali ya kupata mikataba kadhaa ya kufanya maonyesho ya mavazi na ofa ya kusoma nchini Marekani.

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communication, Maria Sarungi ambaye pia ni mratibu wa Taifa wa mashindano hayo, alisema kuwa wanayachukulia matokeo hayo kama changamoto na kuangalia zaidi mashindano yajayo.

“Ni kweli kuwa matokeo yanashangaza, hatujawahi kulalamika katika mashindano ya nyuma, safari hii tulihamasisha wadau watupigie kura nyingi, lakini matokeo ndiyo kama yalivyokuwa,” alisema Maria.

Maria alisema kuwa  wanasubiri kuambiwa lini mrembo ataenda Marekani kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho ya mavazi na mkataba wa kusoma katika fani ambayo ataichagua.
Miss Universe Tanzania (kushoto) akizungumza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere. Anayefuatia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communication, Maria Sarungi na mwakilishi wa Shirika la Ndege la Ethiopia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...