Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstaaf George Mkuchika amewataka Wabunge,madiwani na Viongozi wa Una wanaojihusisha na Biashara Na Halmashauri Kuacha Mara moja kutokana na Kwenda Kinyume na Sheria ya Viongozi Na watumishi wa Uma.
Mkuchika Ameyasema hayo wakati akirejesha taarifa ya fomu za Rasilimali na Madeni katika Ofisi ya sekretarieti ya maadili ya Uma Kanda ya Kusini Iliyopo Mkoani Mtwara.
Mpaka Kufikia Sasa Jumla ya Viongozi 794 ndio wamerejesha fomu za Rasilimali na Madeni kati ya Viongozi 1246 ambao wanatakiwa kuwasilisha.
Aidha Ofisi Hiyo imetenga Siku ya Jumapili tareh 31 kuanzia Mchana mpaka Jioni Kupokea Taarifa kwa Viongozi ambao hawajawasilisha.
Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstafu George Mkuchika Akikabidhi fomu za Rasilimali na Madeni kwa Katibu Msaidizi wa Tume ya serkretariet ya Maadili ya Utumishi wa Uma Kanda ya Kusini Mayina Henjewele.
2.Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt Mstaafu George Mkuchika akionesha fomu Mara baada ya kukabidhi fomu zake na Kuhakikiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...