Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi Leo amefanya Kikao na Waratibu Elimu  Kata 22 wa Wilaya ya Kongwa na idara nzima ya Elimu. Lengo la Kikao hicho ni kufanya tathimini ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.

Katika mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na upungufu wa madarasa,madawati na changamoto nyingine mbalimbali.Pia  kuweka mikakati ya kuondoa changamoto hizo ifikapo muda wa usajili.

Katika kikao hicho Mh. Ndejembi alimuagiza Mkurugenzi kuwasimamisha  kazi waratibu wawili wa Kata ya Njoge na Lenjulu ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zao mbalimbali zinazopelekea kutowajibika vema katika vituo vyao vya kazi.

Mkuu wa Wilaya aliwaasa waratibu hao kuachana na kufanya kazi kwa mazoea (business as usual),  na kuendana na Kasi ya Serikali ya awamu ya tano kwani Mh Rais amewawekea mazingira mazuri ya kazi ikiwemo posho kwa kila MEK Tsh 450,000/= kila mwezi pamoja usafiri. Hivyo wahakikishe  wanatoa huduma bora kwa wananchi.

DC Ndejembi  alieleza kuwa kwa mwaka ujao wa 2018 wanatarajia kusajili wanafunzi wapya wengi sana wa Shule za Msingi na Kidato cha Kwanza kwani Sera ya utoaji Elimu Bure imeamsha Morali zaidi  kwa Wazazi kupeleka watoto Shule.

 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza kwenye Kikao na Waratibu Elimu  Kata 22 wa Wilaya ya Kongwa na idara nzima ya Elimu, Lengo la Kikao hicho ni kufanya tathimini ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...