Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu amezindua mradi wa umeme wa vijijini REA awamu ya pili katika kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni Rufiji Mkoa wa Pwani sambamba na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Naibu Waziri aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo ambapo kwa pamoja waliweza kuzungumza na wananchi hao wakizidi kuwasisitiza kujiunganisha na mradi wa umeme wa REA kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi kwa nishati hiyo muhimu.
Kabla ya kuzinduliwa kwa umeme huo, Naibu Waziri wa Nishati Subira aliweza kupewa taarifa rasmi ya toka kuanza kwa mradi huo wa umeme vijijini REA kutoka kwa Meneja wa TANESCO kutoka Wilaya ya Rufiji Basilus Kayombo ambapo alisema kuwa mradi huo rasmi kwa kijiji cha Mloka ulianza mwaka 2014, na ujenzi wake kuanza 2015 na kumalizika Novemba 2017 na kugharimu takribani bilion 2.5 za kitanzania kutoka Ikwiriri mpaka kufika Mloka.
Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua meadi wa umeme wa vijijini REA, Naibu Waziri wa Nishati ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira, alisema kuwa nia kubwa ya serikali kuleta huduma ya nishati karibu na wananchi ni katika kuchagiza maendeleo yakiwemo wananchi kwa pamoja kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi.
Naibu
Waziri Wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wakati wa ziara
yake ya siku mbili ndani ya Wilaya ya Rufiji na kujionea maendeleo ya
mradi wa umeme vijijini REA ulipofikia na kuwataka wananchi waendelee
kujiunganisha kwa kujaza fomu ili kuweza kupata umeme kwa ajili ya
kuchagiza maendeleo ya kiuchumi ndani ya mkoa wa Pwani.
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Rufiji, Sabilus Kayombo akielezea mradi wa umeme wa vijijini REA katika kata ya Mwasene wenye takribai Kilomita 100 kutoka Ikwiriri ulivyoanza mpaka kufikia tamati Novemba mwaka huu na kugharimu takribani bilioni 2.5 ulioanza kujengwa 2015.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akikagua baadhi Zahanati wakati wa ziara yake ya siku mbili ndani ya Wilaya ya Rufiji.
Wananchi wa kijiji cha Kipo kata ya Kipugila wakionesha malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ya kushindwa kupata umeme wa REA ingawa miundo mbinu ikiwemo nguzo za umeme zimepita katika maeneo yao Kijijini hapo na Naibu Waziri kuwaagiza TANESCO kuweza kuhakikisha kabla hawajaenda kata nyingine wahakikishe vijiji vyote vinne vinapata umeme huo.
Naibu Waziri Wa Nishati, Subira Mgalu akikagua kisima cha maji cha Kata ya Mkongo kinachoendesha kwa nguvu ya rasilimali ga mafuta kutokana na kutokuwa na nishati ya umeme kwenye eneo hilo na kupelekea wananhi kununua maji kwa bei kubwa.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...