Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) na Mkuu wa
Wilaya ya Makete, Veronika Kessy wakiangalia maua ya asili ambayo ni
kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi ya Taifa ya Kitulo wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika
hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni
maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo
hayapatikani kwengineko duniani. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji
kama 'BUSTANI YA MUNGU'.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto), Mkuu wa Wilaya
ya Makete, Veronika Kessy (kulia) na baadhi ya viongozi wa Hifadhi ya
Taifa ya Kitulo wakiangalia maua ya asili ambayo ni kivutio kikubwa cha
utalii katika hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya
Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na
aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko
duniani.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia), Mkuu wa Wilaya
ya Makete, Veronika Kessy na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kitulo,
Pius Mzimbe wakiangalia maporomoko ya maji ya Mwakipembo ambayo ni
kivutio cha utalii ndani ya hifadhi ya Kitulo wakati wa ziara ya kikazi
ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye
wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Pamoja na kivutio hicho hifadhi hiyo
ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo
hayapatikani kwengineko duniani. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama 'BUSTANI YA MUNGU'..
Muonekano mwanana wa Hifadhi
ya Taifa ya Kitulo. Hifadhi hii ina aina zaidi ya 350 za maua huku aina
35 yakiwa ndwele na hupatikana katika hifadhi hiyo pekee duniani.
Vivutio vingine vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ni Maporomoko ya
maji, ndege aina mbalimbali ambao wengine huama kutoka ulaya wakati wa
baridi, wanyamapori aina Swala, Mbega na Nsya. Hata hivyo katika
kutimiza mkakati wa Wizara kuboresha vivutio vya utalii, hifadhi hiyo
ipo katika maandalizi ya kuanzisha makazi ya Pundamilia na wanyama
wengine. Awamu ya kwanza ya kuhamisha pundamiliz 25 kutoka hifadhi ya
taifa ya mikumi inatarajiwa kukamilika mwishoni mw mwaka huu. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama 'BUSTANI YA MUNGU'.
Aina mojawapo ya ua ambalo hupatikana katika hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...