JESHI
la polisi mkoani Tanga, limewahadharisha wananchi kuelekea katika msimu
wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, kujiepusha na vitendo vya
uvunjifu wa amani kama ulipuaji baruti na fataki ikiwemo kuchoma moto
matairi barabarani, kwa yeyote atakayefanya hivyo atachukulia hatua za
kisheri.
Kamanda
mpya wa mkoa huo, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Edward
Bukombe, alisema kwamba jeshi hilo linapiga marufuku kwa mtu yeyote
kulipua au kusababisha milipuko ikiwemo baruti, fataki na Eksozi za
magari, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria namba 13 ya sheria ya
milipuko.
“Hivyo
wakazi wa mkoa wa Tanga, ni marufuku kuchoma matairi hovyo na kulipua
baruti bila kibali, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, kanuni na
taratibu za nchi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakae
kiuka agizo hili,” alisema RPC Bukombe.
Alisema
uzoefu unaonesha kuwa siku za sikukuu watu wengi hujisahau kujiwekea
ulinzi ikiwemo kuwaangalia watoto hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha
wazazi kuhakikisha wanachukua hatua za kuwalinda watoto pamoja na
nyumba zao ili wahalifu wasitumie mwanya huyo kufanya uhalifu wa kuvunja
au watoto kupotea mitaani.
Kamanda
Bukombe alisema kwamba jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa wananchi
wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bali aliwakumbusha
kuzingatia taratibu za kumbi za burudani kufungwa nyakati za saa 6:00
usiku na hata ibada za mkesha wa Krismasi na Mwaka mpya zimalizike muda
huo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto zilikamatwa kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo .
Kamanda
wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa
kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto
zilikamatwa, kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Jeshi hilo Mkoani Tanga,Leonce
na kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo(Habari kwa Hisani ya
Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...