Same
Kaya Saccos yashika nafasi ya pili Mkoa wa Kilimanjaro 2017 kwa
kufanya vizuri katika nyanja zote. Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki
hii wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru ambalo ni
tawi la 2 ukiacha ofisi ya makao makuu Same. A
kizungumza
wakati hafla hiyo fupi iliyofanyika Hedaru, Mwenyekiti wa Saccos hiyo,
Bw. Kisimbo alisema kuwa kwa sasa wametimiza miaka 15 na tayari
wameshapata tuzo siku ya SACCOS dunia mwezi Oktoba 2017.
"Kwa
muda ambao tumekuwa tukiwahudumia wanachama wetu tumeweza kupata
mafanikio mengi likiwemo la kupata tuzo siku ya SACCOS duniani Mwezi
Octoba, 2017," alisema Kisimbo.
Kwa
upande wake Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe.
Rosemary Senyamule aliwapongeza kwa juhudi ambazo wamekuwa wakizifanya
na pia aliwaomba kuendelea kuongeza wanachama wawe wengi zaidi.
Mhe.
Rosemary Senyamule aliwaomba wanachama waendelee kuwa waaminifu kwa
kulipa madeni yao kwa wakati, wananchi wengi kujiunga na SACCOS hiyo
iliyoonyesha mfano mzuri wa kutunza fedha za wanachama wake.

Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto) akionyesha moya ya mashine ya kufulia iliyotolewa na Same Kaya Saccos kwa kituo cha afya cha Hedaru, Kilimanjaro.

Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akiwa amenyanyua mikono mara baada ya kukata upete wa kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru, Kilimanjaro.

Watoto yatima na wa mazingira magumu Hedaru wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rosemary Senyamule mara baada ya kupatiwa zawadi ya madaftali.

Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wakati wa hafla hiyo.
Mhe. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Same Kaya Saccos.

Watoto yatima na wa mazingira magumu Hedaru wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rosemary Senyamule mara baada ya kupatiwa zawadi ya madaftali.

Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wakati wa hafla hiyo.

Mhe. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Same Kaya Saccos.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...