Desemba 2, 2017 katika chuo kikuu cha Mt. Augustine (SAUTI) Mwanza kulifanyika tamasha la uvumbuzi, ujasiriamali na kazi kwa wasichana lijulikanalo kama PANDA. Tamasha hilo ambalo huandaliwa kila mwaka na taasisi ya wasichana iitwayo Her initiative, inayojikita katika kumsaidia msichana kuweza kusimamia maswala yake binafsi, kifedha, kielimu, na kumpa uelewa msichana katika Nyanja mbali mbali za ujasiriamali wakiwa vyuoni. 

Kwa mara ya kwanza taasisi hiyo (her initiative) iliamua kufanya tamasha hilo jijini Mwanza ikiwa ni msimu wa nne kufanyika tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo, huku dhamira ya msimu wake huu wanne ilikua ni Uvumbuzi kwenye kila idara. 

Tamasha hilo lilihudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 800 kutoka vyuo vikuu na Taasisi za elimu mbali mbali zilizopo jijini Mwanza ikiwemo CBE, CUHAS na Mzumbe. Wasemaji wakuu katika tamasha hilo kwa mwaka huu walikuwa ni Benjamin Fernandes Mtanzania wa kwanza kupata nafasi ya kusoma Vyuo vikuu bora marekani vijulikanavo kama STANFORD GRADUATE SCHOOL OF BUSINESS na HAVARD KENNEDY SCHOOL OF GOVERNMENT na pia kufanya kazi katika foundation kubwa ya kimataifa ijulikanayo kama Bill and Melinda Gates. Ambaye aliongelea Uvumbuzi katika nafasi za kimataifa. 

Idris Sultan mshindi wa BBA, mchekeshaji , mtangazaji na Balozi wa Global Peace. Ambaye aliongelea maswala ya uvumbuzi katika Sanaa na kipaji na kushirikisha story yake binafsi ya mafanikio. 

Rose Ndauka mjasiriamali na mshindi wa kike wa tuzo za uigizaji , muanzilishi wa Ndauka Advert na mmiliki wa Connexion House of Beauty  Dar es salaam alieongelea Uvumbuzi kwenye Sanaa, biashara. 

“Muamko huu wa wanafunzi wengi zaidi ya 700 inaonyesha jinsi gani  vijana wa sasa walivo na nia ya kutaka mafanikio na kujifunza njia mbali mbali za ujasiriamali na uvumbuzi naamini kupitia wazungumzaji wa leo vijana hakika watakua wamebadilishwa kifkra. Tumeona umuhimu wa tamasha hili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hivyo tunategemea kufanya Zaidi na mikoa mingine “  Alisema mwenyekiti wa taasisi hii ya Her initiative Maureen Richard. 

Panda 2017 Mwanza imedhaminiwa na TECNO mobile Tanzania, Jembe FM na Michuzi Blog.
  Mchekeshaji na Mshindi wa Big Brother Afrika 2014,Idris Sultan akizungumza leo katika semina ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza.
Msemaji na Muhamasishaji katika fursa za kimataifa, Benjamin Fernandes akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya jijini Mwanza kwaajili ya kuwavutia kwa njia mbalimbali kutokana na aliyoyapitia katika maisha ya shule pamoja na maisha ya Kawaida.Pia amewashauri wanafunzi hao wa vyuo vikuu vya jijini Mwanzakusoma kwa bidii pamoja na kuwa wavumilivu kwenye vikwazo mbalimbali wanavyokutana navyo. Hayo yamesemwa katika semina fupi ya kuwashawishi iliyoandaliwa na Taasisi ya her initiative Present PANDA iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza.
 Msanii wa Bongo Muvi na Mjasiriamali na mshawishi katika upande wa sanaa, Rose Ndauka akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza katika semina iliyofanyika leo katika chuo kikuu cha Makatifu Agustino jijini humo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Her Initiative - PANDA, Moureen Richard akizungumza na katika semina ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza.
Baadhi ya wananfunzi wa vyuo vikuu vya jijini Mwanza wakiwasikiliza watoa maada katika semina iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Augustino jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...